Rais Samia atia wino miswada minne ya sheria

By Dotto Charles , Nipashe
Published at 01:14 PM Apr 02 2024
Rais Samia Suluhu Hassan.
PICHA: IKULU
Rais Samia Suluhu Hassan.

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesaini miswada minne ya sheria iliyopitishwa na Bunge na hivyo kuwa sheria.

Akizungumza bungeni leo April 2, 2024, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ametaja miswada iliyosainiwa ni Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, na Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa, Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa na Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Kwa mujibu wa Spika Tulia, sasa sheria hizo sasa zitatambulika kama Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na.2 ya mwaka 2024, Sheria ya Markebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 3 ya 2024 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na.4 ya mwaka 2024.