Kunenge aagiza Mkuranga kupanga maeneo ya uwekezaji na makazi

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 08:29 PM Jul 26 2024

MKUU  wa mkoani Pwani, Abubakar Kunenge.
Picha: Julieth Mkireri
MKUU wa mkoani Pwani, Abubakar Kunenge.

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ametoa maagizo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuhakikisha wanapanga mji huo maeneo ya uwekezaji na makazi Ili kuepusha migogoro ya wananchi na wenye viwanda.

Kunenge ameyasema hayo Julai 26 alipofanya ukaguzi katika kiwanda cha kutengeneza kioo cha KEDA kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Amesema Ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara ni vema halmashauri hiyo ikawa na mpango wa kupima viwanja na kuweka halmashauri hiyo katika mpangilio mzuri.

Kadhalika amezielekeza taasisi wezeshi kuondoa vikwazo kwa wawekezaji badala yake watumie nafasi zao kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa ili kufikia malengo waliyowekwa.

Kunenge amepongeza uwekezaji wa Kiwanda hicho ambacho hadi kukamilika kinataajia kugharimu dola za kimarekani milinon 309 sawa na fedha ya kitanzania sh.bilioni 803.4.

1

Vilevile Kunenge amejinasibu kuwa ongezeko la viwanda mkoani humo litaongeza uzalishaji wa bidhaa na malighafi hali itakayosaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo nje ya nchi.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Ofisa biashara Ruby Zhu amesema ujenzi wa mradi huo ulianza 2023, na upo awamu kwanza ambapo utakamilika baada ya miezi 18 na awamu ya pili itaanza mwaka 2027.

Zhu amesema uzalishaji wa bidhaa hizo utaanza mwezi Septemba ambapo watazalisha tani 600 na kwa mwaka watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 219.

Kwasasa Mkoa wa Pwani una viwanda 1,535 ambapo viwanda vikubwa ni 124 na vingine vidogo na vikubwa huku kiwanda hicho kikiwa ni cha pili kwa uzalishaji wa kioo kwa Mkoa wa Pwani.
2