Suala la miundombinu rafiki wenye ulemavu si mjadala
TAASISI za umma na binafsi nchini zimekuwa zikifanya ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya sekta kadhaa kama vile elimu, afya, uchukuzi na usafirishaji na nyumba za makazi. Lengo la kujenga miundombinu hiyo ni kuwaondolea wananchi kero na kuleta ufanisi katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya wadau na taifa kwa ujumla.