Prof. Mkenda afafanua sababu kuahirishwa mtaala mpya kidato cha tano

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 08:56 PM Jul 26 2024

Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Picha: Mtandao
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amefafanua sababu zilizofanywa kuahirishwa kwa utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa wa kitado cha tano mwaka 2024/2025 ni pamoja na vitabu vya kufundishia kutochapishwa na uhaba wa waalimu wa baadhi ya masomo ya lazima ikiwemo somo la ujasiriamali.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Ijumaa 26,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ambapo  amesema wameamua kuahirishwa kwa mtaala huo hadi mwakani ili kupisha maandalizi yote kukamilika.

“Katika maeneo mengine yote mtaala mpya unaendelea ktekelezwa kwanzi darasa la kwanza,la pili na la tatu lakini huku kwenye masomo ya kidato cha tano kuna vitu ambavyo bimeonekana kuwa havija kamilika ikiwemo vitabu bado havija chapishwa vya mtaala mpya.

“Tumeona kama tutaanza sasa kuprint vitabu vya masomo ya mtaala huu mpya hatuta maliza kwa wakati hadi kivisambaza lakini kuna baadhi ya shule alitaka wapewe soft copy lakini wengine  wakasema kuwa hawaeezi kuchapisha hivyo tukaona hatuwezi kuwa na mtihani ambao shule zimetumia mitaala tofauti hivyo basi tumeahirisha hadi mwakani”amesema