Kigogo ACT Wazalendo akerwa na huduma mbovu za afya Kondoa

By Sabato Kasika , Nipashe
Published at 09:04 PM Jul 25 2024
NAIBU Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa,  Shangwe Ayo.
Picha: Mpigapicha Wetu
NAIBU Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Shangwe Ayo.

NAIBU Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Shangwe Ayo amesema huduma mbovu za afya zinawatesa akinamama wa wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Amesema, wanatozwa faini ya shilingi 50, 000 wanapojifungulia nyumbani kwa bahati mbaya, na kwamba hata kama watajifungulia hospitalinim bado wana tozwa zaidi ya shilingi 50,000, kwa ajili ya kujifungua. 

Naibu mwenezi huyo amesema hayo leo, katika mkutano wa hadhara akiwa Kondoa katika ziara ya viongozi wa chama inayofanyika mikoa mbalimbali nchini. "Serikali ina sera ya afya ya mama wajamzito lakini imeshindwa kufanya kazi, matokeo yake ni wajawazito kuteseka," amesema Shangwe.

Amesema, serikali Haina budi kufuatilia kwa karibu huduma za afya zinazotolewa katika hospitali za umma ili kuoma kama zinaridhisha.

"Bila wizara kuchukua za makusudi, Watanzania hasa akinamama wataendelea kuteseka kwa huduma mbovu. Yaani wizara iache kutesa akimama wajawazito kwa kuwanyima huduma bora za afya," amesema.