Watanzania, Wakenya waungana kuiombea Kenya

By Neema Emmanuel , Nipashe
Published at 08:48 PM Jul 26 2024
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda.

WATANZANIA wameungana na Wakenya kufanya maombi ili nchi hiyo iwe na amani kama Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda alipokuwa akizungumza na wananchi walioudhuria mkutano wa Mwinjilist Ezekiel Odero wa Kanisa la Newlife Prayer Center and Church kutoka Mombasa nchi Kenya.

RC Mtanda, amesema Watanzania na Wakenya ni ndugu hivyo mmoja akipata matatizo ni lazima tuungane kuwaombea matatizo yaishe.

Amesema wanaimani Mwinjilist Ezekiel ataendelea kuliombea Taifa la Kenya na azidi kuwaombea Watanzania ili waendelee kuwa na amani waliyonayo na Mwenyezi Mungu azidi kuizidisha amani hiyo. 

1


" Mwinjilist Ezekiel umefika hapa umeona amani ipo tele tunamshukuru sana Rais kwa kuimarisha amani, upendo na mshikamano nawaomba Watanzania waendelee kuilinda amani hii ikipotea hawataweza kuendelea kumwabudu Mungu ipasavyo sisi kama serikali ya Mkoa wa Mwanza tutaendelea kukupa ushirikiano mkubwa hadi siku utakapokamilisha kutoa huduma " ameeleza Mtanda.

Aidha ameeleza kuwa watu wote waliojitokeza wanahitaji maombi ili wapate kufunguliwa na kuponya hiyo ni kutokana na imani waliyonayo juu yake , tumeshuhudia miujiza mahali hapa hivyo serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mungu ambao watapenda kutoa huduma mkoani hapo.

Naye Mwinjilist Ezekiel Odero ameeleza kuwa uwa anaiombea nchi yake karibu kila siku na Mungu ajalisahau Taifa la Kenya pia Watanzania watambue kuwa kuna dhahabu ambayo wanayo na inathamani kubwa sana uwezi ipata kirahisi anaomba wailinde ambayo ni amani na upendo.
2