Serikali yaanza kuchunguza watumishi mapenzi jinsia moja

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 07:12 PM Oct 17 2024
Serikali yaanza kuchunguza watumishi mapenzi jinsia moja
Picha:Mtandao
Serikali yaanza kuchunguza watumishi mapenzi jinsia moja

OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwapo kwa viashiria vya mmomonyoko wa maadili kinyume na mila na desturi vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Aidha, Ofisi hiyo imekuwa ikipokea mrejesho kutoka kwa wananchi wanaohudumiwa kuhusu hali isiyoridhisha ya mavazi kwa watumishi wa umma. 

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Xavier Daudi aliyasema hayo leo Oktoba 17,2024 jijini hapa kwenye ufunguzi wa kikao kazi baina ya ofisi hiyo, taasisi zinazosimamia maadili na mamlaka zinazosimamia maadili ya kitaaluma. 

Amesema vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini pia ni vitendo vya kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.