Rais Samia amaliza mgogoro wa uliodumu zaidi ya miaka 30 kati ya kanisa na serikali

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 05:39 PM Oct 17 2024
Rais Samia amaliza mgogoro wa uliodumu zaidi ya miaka 30 kati ya kanisa na serikali
Picha:Mpigapicha Wetu
Rais Samia amaliza mgogoro wa uliodumu zaidi ya miaka 30 kati ya kanisa na serikali

Rais Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kurejeshwa kwa eneo la takribani mita za mraba 7503 na Sh. Milioni 500 zilizokuwa mali ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto wa Yesu lililopo Jijini Arusha.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Paul Makonda, wakati akikabidhi hati kanisani hapo amesema hatua hiyo imefikiwa mara baada ya mgogoro huo wa miaka zaidi ya 30 kati ya Kanisa hilo na serikali kumfikia Rais na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa.

Amesema serikali ililichukua eneo hilo kinyemele na baadae kulitaka kanisa hilo kutoa Sh  Milioni 500 za kulipia eneo hilo wakati walipokuwa na mpango wa kuongeza eneo la huduma kanisani hapo.

Naye Mhashamu Baba Askofu, Dk. Isaac Amani, Askofu wa Jimbo kuu Katoliki la Arusha, amemshukuru Rais Samia kwa kuwa mtatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi.

Aidha, amekemea ubinafsi, Ubabe, kutojali maendeleo ya wengine na ulafi kwa baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu nchini.