Baraza la Mitume na Manabii wajitosa kuchochea amani

By Neema Emmanuel , Nipashe
Published at 07:51 PM Jul 25 2024
 Rais wa Baraza hilo Dk. Nabii Joshua Mwantyala.
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais wa Baraza hilo Dk. Nabii Joshua Mwantyala.

BARAZA la Mitume na Manabii Tanzania ( BACCT ) watoa ahadi ya kuwa wachochezi wa amani kwa kuhamashisha umoja na mshikamano ili kuilinda na kuepuka mgawanyiko.

Hayo wamebainishwa na Rais wa Baraza hilo Dk. Nabii Joshua Mwantyala mara baada ya kumaliza mkutano wa Mwinjilist Ezekiel Odero wa Kanisa la Newlife Prayer Center and Church kutoka Mombasa nchini Kenya wa siku ya kwanza anaeleza kuwa wao kama viongozi wa kiroho wanaowajibu wa kuiombea nchi.

Anaeleza wameshuhudia mataifa mengi duniani wana migogoro ikiwemo ya kisiasa,kijamii na kikabila hivyo Baraza limeandaa mpangilio maalum wa kuliombea Taifa
lengo kubwa ni kuhubili Injili ya Bwana  Yesu Kristo na kuisaidia jamii ya Tanzania kwa kumuombea Rais .

"Nchi yetu inazidi kuwa na amani naamini kwa miaka mingi Tanzania imeonekana ni sehemu sahihi na bora zaidi kuishi binadamu kwa sababu ya amani ,Mitume na manabii wa Tanzania tumechagua kuwa wachochezi wa amani hiyo ambayo Mungu ametupatia kwa kuiombea nchi na viongozi hususani kipindi hiki tunachotarajia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kama hatuwezi kuwahamasisha watanzania  kuwa wa moja nchi inaweza kugawanyika  " anaeleza.

1

Anaongeza kuwa wamekusudia kutimiza wajibu huo kwa ushirikiano na mgeni wao Mwinjilist Ezekiel pamoja na mkewe Sarah kwa kutumia mikutano hiyo mikubwa inayogusa maisha ya watu  kiroho kuhamasisha umoja, mshikamano ili kulinda amani hiyo .

"Rais amefanya kazi kubwa tangu alipopokea nchi hii tukiwa na msiba mkubwa kwa ujasiri mkubwa na hekima Mungu aliyompa tunazidi kuwa na amani hata kwa kipindi hicho kigumu na ametekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo wengi waliamini haiwezi kutekelezeka pia ametuonyesha mwanamke anaweza kufanya jambo kubwa akiamua kwa sababu mungu akimbaliki yeyote anaweza kufanya makubwa." anasema na kuongeza kuwa.
Kwa kazi kubwa hiyo anayoifanya tunawajibika kumwombea neema na baraka Mungu ampe uwezo zaidi ikiwezekana ampe kibari cha kuendelea kuongoza nchi yetu kwa miaka mingine .

2