Helkopta mbili za Jeshi zagongana na kuua watu 10

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:40 PM Apr 23 2024
Helkopta za Jeshi zagongana Malaysia.
PICHA: MAKTABA
Helkopta za Jeshi zagongana Malaysia.

WATU kumi wamefariki dunia baada ya helikopta mbili za jeshi la wanamaji kugongana angani wakati wa mazoezi ya kijeshi ya gwaride la Wanamaji wa Kifalme Malaysia.

Helikopta mbili za kijeshi za Malaysia zimegongana na kuanguka wakati zikifanya mazoezi angani mapema leo na kuwaua watu 10 waliokuwamo ndani yake.

Picha zilizosambaa mtandaoni zilionesha helikopta kadhaa zikiruka usawa wa chini kwa mpangilio katika uwanja wa jeshi la wanamaji, wakati zikifanya mazoezi kabla ya sherehe ya jeshi hilo mwezi ujao.

Baadaye ndege hizo ziligongana na kuanguka na kusababisha vifo vya watu 10. Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa akisema kuwa taifa linaomboleza msiba huo mkubwa.

Mwezi uliopita, helikopta moja ya walinzi wa pwani ya Malaysia ilianguka kwenye mlango bahari wa Malacca. Mwaka 2016, naibu waziri alikuwa miongoni mwa watu waliofariki baada ya helikopta kuanguka katika jimbo la Sarawak nchini Malaysia.

DW