Wanaodaiwa kumuua mtoto Grayson wapandishwa kizimbani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:06 PM Dec 30 2024
Wanaodaiwa kumuua mtoto Grayson wapandishwa kizimbani

Watuhumiwa wawili wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Mfanyabiashara Dodoma Grayson Kanyenye (6) anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani, na mwili wake kukatwa na kitu chenye ncha kali, maeneo ya Ilazo Extention jijini Dodoma wamefikishwa mahakamani Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Dodoma leo Disemba 30, 2024.