Watu wenye ulemavu 188 wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, ikiwamo yasiyoambukiza kama vile kisukari na presha.
Matibabu hayo yamefanyika wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana na zawadi kwa makundi hayo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo JKCI, Dk. Mohamed Aloyce, alisema katika upimaji huo watu wenye ulemavu 20 wamepewa rufani kufika katika tawi la taasisi hiyolililopo Kawe, kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Tumewakuta baadhi ya watu wana matatizo ya shinikizo la juu l a damu, lakini kutokana na vipato vyao kuwa chini wanashindwa kwenda hospitali, kwa ajili ya matibabu ama hata wakienda na kupewa dawa mara moja hawarudi tena,” alisema Dk. Aloyce.
Bingwa huyo alisema kupitia hafla hiyo watu wenye ulemavu wamepata huduma za afya, ingawa bado kuna mahitaji ya wao kuwa na bima ya afya, kwa kila mmoja, ili pale wanaopopata changamoto za afya waweze kutibiwa kirahisi, ni makubwa.Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Stevene Mengele, alisema taasisi hiyo imewakusanya watu wenye ulemavu kukaa nao pamoja na kuwapa faraja.
Stevene alisema kundi la wa lemavu husahaulika ndio maana baada ya kuwakusanya wakaona kuna umuhimu wa kupimwa magonjwa ya moyo, kucheza nao pamoja na kuwapa faraja, ili wajisikie kuwa sawa na wengine.
Stevene aliwapongeza wataalamu wa afya, kwa kuwa na moyo wakujitoa kwa watu hao kuhakikisha wote waliohitaji huduma ya uchunguzi wa afya wamepata kwa wakati.
“Kazi ya kutibu ni ngumu, Mungu awasimamie, tunaomba sana msituache hata hapo baadaye tukiwataka tena mtukubalie, ili kwa pamoja tuweze kuwafikia watu wa kundi hili, kupata huduma hizi muhimu za afya,” alisema Stevene.
Wakiongea mara baada ya kupima afya, wameishukuru serikali kwa kutoa huduma hiyo kwao kwani wengi wao hawakuwahi kufanya vipimo kama hivyo na hawakuwa na matarajia ya kupima moyo katika maisha yao.Joseph J ackson, mkazi wa Mbagala, alisema hakujua kama ana tatizo la kisukari, hadi alipopima na kupata majibu katika hafla hiyo.
“Naishukuru sana serikali yangu kwa kutusaidia kupata huduma za afya, leo nimepima magonjwa ya moyo, sukari, na shinikizo la damu na kukutwa na tatizo la sukari. nimepewa rufaa na nina ahidi kwenda kuchunguza zaidi.
Agnes Mwanuke, mkazi wa Temeke, ameishukuru JKCI kwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa walemavu, kwani amekuwa wakisikia maumivu makali upande wa kushoto wa moyo lakini kutokana na utafutaji wake, kuwa mgumu hakufikiria kwenda hospitali kutibiwa.
“Sisi watu wenye ulemavu utafutaji wetu ni washida sana hivyo kushindwa kupata kipato cha kutupeleka hospitali kupata huduma za matibabu, lakini walivyotusogezea hapa tunawashukuru sana kwani tumechunguza afya zetu,” aliema Agnes.
Aliomba huduma hizo zisiishie kwao tu, hao bali taasisi iangalie namna ya kuwafikia wenye walemavu wengine nchini, ili nao waweze kupima afya zao kwani afya ndio mtaji wa maisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED