Wizara ya Afya imetoa wito kwa mkandarasi Kiunga Builders kuongeza kasi ya ujenzi wa Mradi wa Maabara ya Kisasa inayojengwa katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe chini ya Ufadhili wa Global Fund.
Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Afya, Seth Akyoo ametoa wito huo leo alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo jijini hapa.
Akyoo amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Maabara hiyo ya Kisasa utagharimu kiasi cha sh.Milioni 800 na itakapokamilika itaboresha huduma za uchunguzi katika Hospitali hiyo na kuleta ufanisi.
Naye, Msimamizi wa Mradi kutoka Kiunga Builders, Mhandisi Jackson Kitundu ameahidi kuzingatia maelekezo hayo ya Wizara ili mradi ukamilike ndani ya muda uliopangwa Agosti 3, mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED