Tazama hapa matokeo: Wasichana vinara darasa la nne, kidato cha pili

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:50 PM Jan 04 2025
 Wasichana vinara darasa la nne, kidato cha pili wavulana waongoza.
Picha:Mtandao
Wasichana vinara darasa la nne, kidato cha pili wavulana waongoza.

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetoa matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili, huku wasichana wakiwa vinara wa ufaulu kwa darasa la nne na wavulana wakiongoza kidato cha pili.

Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 4, 2025 na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed.

Jumla ya wanafunzi 1,320,227 kati ya wanafunzi 1,530,911 waliofanya mtihani wa darasa la nne, sawa na asilimia 86.24 wamefaulu kwa kupata madaraja A, B, C na D ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.9.

Aidha kati ya waliofaulu, wasichana ni 699,901 sawa na asilimia 53, na wavulana ni 620,326 sawa na asilimia 47.

Vilevile kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu kuendelea na kidato cha tatu, wasichana ni 367,457 na wavulana ni 313,117.

DARASA LA NNE https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/sfna/sfna.htm

KIDATO CHA PILI https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/ftna/ftna.htm