Balozi afutwa kazi madai kutaka wafanyakazi wa kiume kumnyoa sehemu za siri

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:40 PM Jan 06 2025
Baalizi Mazuba Monze.
Picha: Mpigapicha Wetu
Baalizi Mazuba Monze.

Rais wa Zambia amemfuta kazi Balozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini kwa utovu wa nidhamu, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amechukua uamuzi huo baada ya Baalizi Mazuba Monze, kuripotiwa kutaka wafanyakazi wake wa kiume kumnyoa sehemu za siri.

Mwanadiplomasia huyo ambaye alikuwa akihudumu katika ubalozi wa Zambia mjini Pretoria ameripotiwa kutoa ombi lisilo la kawaida, na agizo lisilo la kawaida, Mazuba anatajwa kuwataka wafanyakazi kumnyoa sehemu zake za siri ambapo wafanyakazi hao walikataa, wakisema kuwa haikuwa sehemu ya majukumu yao kumnyoa balozi hasa sehemu za siri.

Balozi alichukulia kitendo hicho kuwa ni kutotii na hivyo kupelekea kuwafuta kazi wafanyakazi, hata hivyo baada ya ukimya wa muda mrefu wafanyakazi walikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na kulifikisha suala hilo kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wakati madai kuhusu matakwa hayo yaliyoshangaza wengi ya Monze yalipothibitishwa, Rais Hakainde Hichilema alimfuta kazi mara moja balozi huyo wakati huo huo ripoti nyingine zinasema kuwa madai dhidi ya Monze yametiwa chumvi.

Gazeti la Maravi Post linaripoti kuwa raia wa Zambia anayeishi Afrika Kusini amejitokeza, akidai kuwa madai dhidi ya Monze huenda yametiwa chumvi au kutungwa na wapinzani wake, Mtu huyo anadai kuwa kampeni ilizinduliwa dhidi ya Monze, ikihusisha ripoti za uongo na uzushi, ambao hatimaye ulisababisha kufukuzwa kwake.

Wakati haya yote yakiendelea, bado inabakia kusuburiwa ni hatua gani zaidi zitachukuliwa na matokeo gani Monze atakabiliana nayo, hata hivyo jambo moja ambalo ni hakika ni tukio hilo limeacha doa kwa sifa ya kidiplomasia ya Zambia na kuibua maswali juu ya mwenendo wa wawakilishi wake nje ya nchi.