“Gwamaka yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi yake”-Polisi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:55 PM Jan 06 2025
Gwamaka Francis Gehas.
Picha:Mtandao
Gwamaka Francis Gehas.

Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kupatikana kwa Mtangazaji wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas,maarufu kama Boiboi Mkali mkazi wa Mbezi Beach African, Dar es Salaam, aliyedaiwa kupotea mapema Januari 3, 2025 amepatikana akiwa kwa shangazi yake Kitunda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, iliyotolewa jana Januari 5 imebainisha kuwa baada ya ufuatiliaji ulioanza kwa kukusanya ushahidi na taarifa kutoka kwa watu mbalimbali,jana walipokea taarifa kutoka TV 3 kuwa Gwamaka yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi yake.

Aidha Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake ili kujua uhalisia wa tukio la kutokuonekana kwake na baadaye kuonekana akiwa kwa shangazi yake.

Kusoma habari hii zaidi tembelea epaper.ippmedia.com

#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital