MAZOEZI ya mwili, sio lazima kiafya yanatajwa yawe magumu. Hata kutembea haraka kwa dakika 10 kwa siku, kunatajwa kuwa na manufaa mbalimbali ya afya.
Inatajwa kupunguza hatari ya magonjwa mbalimbali, ikiwamo ya moyo, kiharusi na baadhi ya kisaratani.
Inatajwa kitaalamu kwamba, mabadiliko machache kwenye jinsi mtu anavyotembea, yanaweza kubadilisha mazoezi hayo kuwa rahisi na yakifanyika kila siku, kwa manufaa zaidi kwa afya ya mtembeaji.
Ikiwa mtu anapenda kupata faida zaidi kiafya, kutokana na matembezi yako, hapo kuna njia tano za kuyafanya kuwa ya manufaa zaidi:
Mosi, tofautisha kasi: Njia mojawapo inayoongeza faida za kutembea ni kubadilisha kasi ya kutembea, badala ya kudumu katika mwendo uleule.
Pia, mtu anatakiwa kujumuisha vipindi vya kutembea haraka, ikifuatiwa na polepole.
Mbinu hiyo inajulikana kama kutembea kubadilisha kasi kwa vipindi, kwamba kunaboresha utendaji wa moyo na mishipa yake kwa ufanisi zaidi, kuliko kutembea kwa kasi isiyobadilika.
Utafiti uliofanywa kwa miezi minne, kupishana kwa dakika tatu za kutembea haraka na dakika tatu za kutembea kwa mwendo wa wastani, kulionyesha maboresho makubwa zaidi katika udhibiti wa sukari ya damu na viwango sawa vya mwili.
Hiyo inatajawa ni kwa watu wazima walio na ugonjwa wa kisukari cha aina ya pili, kuliko waliotembea kwa miguu kila mara, wakiwa na kasi sawa.
Kutembea kwa muda, pia husababisha kupunguzwa mafuta mwilini na kunaboresha ukakamavu, pia ustahimilivu wa jumla mwilini.
Ili kujumuisha hili katika matembezi yako ya kila siku, mhusika anashauri ajaribu kuongeza mwendo wako kwa dakika chache, kisha anarudi kwenye kasi yake ya kawaida.
Ni jambo linalofanyika kwa kurudia mzunguko huo wa matembezi, ili kuongeza mapigo ya moyo na kuchoma kalori zaidi.
Pili, tembea kwa mwendo kasi,kutembea haraka sio tu ya kunakufikisha unakoenda mapema, pia ni njia inayoleta faida zaidi kiafya.
Takwimu zilizochambuliwa kwa zaidi ya watu 50,000 wanaotembea, iligundulika kuwa mwendo wa angalau maili tatu kwa saa, ulihusishwa na kupunguza hatari ya kifo kutokana na sababu kadhaa
Hapo imajumuisha hatari ya chini ya kifo kutokana na ugonjwa wa moyo na mishipa, pia maradhi ya saratani.
Watafiti pia, wameonyesha kwamba, kuongeza kasi ya kutembea, kunaweza kuboresha afya ya moyo ya mtu na kusaidia kudhibiti wa uzito.
Mtu anatajwa akiwa hana uhakika kuhusu mwendo wako, ajaribu kutembea kwa kasi ambapo unapumua haraka zaidi, lakini bado anaweza kufanya mazungumzo.
Tatu, kuongeza uzito wa kubeba: Mtu anapobeba mzigo au uzani wa ziada wakati wa kutembea, kunaweza kumwongezea nguvu ya mazoezi.
Kwa kuvaa fulana au mkoba wenye uzani, kunalazimisha misuli yako kufanya kazi kwa bidii zaidi - kuongeza nguvu na kuchoma kalori zaidi.
Inatajwa, mtu anapotaka kujaribu, ni muhimu akaanza na uzito mdogo, ili kuepuka matatizo au majeraha.
Tafsiri ya uzani huo, unaanzia kwenye mavazi kama fulana au mkoba, unaowakilisha asilimia tano ya uzito wa mwili wake.
Mtu mwenye uzani wastani kwa mfano kilo 80, anaweza kuanza kwa kuongeza kilo nne pelee, ukiwa uzani wa ziada kwenye mkoba wake.
Kwa hatua, akaongeza kiwango cha uzito unaobeba kadiri unavyojisikia vizuri zaidi na ahakikishe uzito unabebwa, unasambazwa sawa, ukidumisha mkao mzuri wakati mtu anatembea (usielemee, ukande mmoja).
Nne, safari ipitie milima au ngazi: Kuchagua mwelekeo unaofaa kwenye matembezi, kunasaidia kuleta mabadiliko makubwa safarini.
Matembezi kwenye milima au ngazi, kunashirikisha sehemu tofauti ya misuli, hasa miguuni, ikilinganisha kutembea kwenye ardhi tambarare.
Hii sio tu huongeza nguvu, pia anachoma kalori zaidi, kwani kutembea kwa miguu na huongeza kasi ya mazoezi yake, bila kuhitaji kutembea haraka.
Zaidi ya hayo, huwa anatembea chini, pia inaboresha kazi ya misuli na uthabiti wa mwili wako.
Tano, inatajwa haja ya mtu kujizoesha kutembea kwa uangalifu.Jinsi ya kuanza hapo, napo panaelezwa kutembea hakuishii kw manufaa ya kimwilini, pia kunaweza kuboresha ustawi wako wa akili wa mtu.
Tafsiri inayotolewa ni kwamba, kunahusisha kuzingatia kwa makini mwenendo, kupumua na mazingira yaliyoko.
Inarajewa kuwapo utafiti unaoonyesha kuwa watu waliofanya mazoezi ya kutembea kwa uangalifu kila mara, kwa walau mwezi mmoja.
Hapo walishuhudia kupunguza viwango vya mfadhaiko na maboresho kwa afya yao ya akili kwa ujumla.
Mtu anashauriwa kutembea kwa uangalifu, akianza kwa kuzingatia hisia za kila hatua, mdundo wa anavyopumua, pia sauti zinazokuzunguka.
Inatajwa kuboresha afya ya akili, huku matembezi yakifanywa kuwa ya kufurahisha zaidi na kinachifuata zaidi ni; kuongeza mielekeo kwenye matembezi, kwa dhumuni ya kuleta mabadiliko makubwa.
NAMNA KUANZA MAZOEZI
Jinsi ya kuanza: Inatajwa suala la kuboresha matembezi yako hakuhitaji mabadiliko makubwa, lakini kuna mambo machache unapaswa kukumbuka ili kukaa salama, kupunguza hatari yako ya kuumia, na kuongeza manufaa:
Pasha joto na punguza mwendo: Anza na dakika chache za kutembea kwa urahisi ili kupasha misuli joto. Maliza matembezi hayo kwa kupunguza mwendo na umalize kwa kunyoosha taratibu ili kuupoza mwili wako.
Vaa viatu vinavyofaa: Chagua viatu vizuri na usaidizi mzuri ili kuepuka majeraha.
Tembea na maji: Lete maji, haswa unapotembea kwa muda mrefu au katika hali ya hewa ya joto, ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.Sikiliza mwili wako: ikiwa unahisi maumivu au usumbufu, punguza kasi au pumzika. Ongea na daktari wako ikiwa shida inaendelea.
Hatua kwa hatua ongeza kiwango: Ikiwa unaongeza uzito, kukabili vilima, au kuongeza kasi, fanya hivyo hatua kwa hatua ili kuruhusu mwili wako kubadilika.
Hiyi inamaanisha kufanya mazoezi ya ziada kidogo kila wakati, ili kutathmini jinsi mti anaavyohisi.
Kwa ujumla, kunaelezwa kutembea ni njia nzuri ya kuboresha na kudumisha afya ya mwili, hatua inayoenda na kufanyika marekebisho madogo kwenye mwendo huo
Hilo lifanyika, ndani ya tabia ya utembeaji wa kila siku, huku kisakilijia ikiwa ni njia ya bora na inayofurahisha.
Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED