Wachezaji 6 wanaowania uchezaji bora EPL 2023-24

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:22 AM Apr 01 2024
Declan Rice.
Picha: Getty
Declan Rice.

KAMPENI ya Ligi Kuu England ya 2023-24 imekuwa ya aina yake. Arsenal, Liverpool na Manchester City zote zipo katika vita ya farassi watatu kuwania taji la Ligi Kuu England. Ni wachezaji wachache tu ambao wameweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu mara mbili katika maisha yao ya soka kwenye ligi hiyo.

Orodha ya wachezaji hao ni pamoja na Thierry Henry, Cristiano Ronaldo, Nemanja Vidic na Kevin De Bruyne, na Ronaldo pekee ndiye aliyeshinda katika miaka miwili mfululizo (2007 na 2008).

Huku msimu wa Ligi Kuu ya 2023-24 ukielekea mwishoni, hebu tuwatazame wachezaji sita wanaowania taji la mchezaji bora wa msimu huu...

 #6. Mohamed Salah (Liverpool)

Mchezaji bora wa msimu wa 2017-18 atalenga kuongeza taji la pili la Ligi Kuu na tuzo binafsi kwa mara ya pili. Salah bado ana mabao 15 na asisti tisa katika mechi 22 alizocheza hadi sasa kabla ya mechi za wikendi.

Raia huyo wa Misri atakuwa akiwania Kiatu cha Dhahabu ambacho ni cha nne kwa rekodi katika Ligi Kuu England huku akiwa amefunga mabao matatu nyuma ya kiongozi wa ligi hiyo, Erling Haaland. Salah angeorodheshwa juu zaidi kama asingekuwa majeruhi baada ya kupata jeraha wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast mapema mwaka huu.

Hakuna shaka kuwa Salah ni mmoja wa wachezaji bora kuwahi kuichezea Liverpool. Lakini ikiwa anaweza kuiongoza Liverpool kutwaa taji lingine la ligi pamoja na tuzo ya pili ya mchezaji bora, atakuwa kwenye daraja la juu kama mmoja wa wachezaji bora wa wakati wote wa Ligi Kuu England.

 #5. Erling Haaland (Manchester City)

Haaland alikuwa na nafasi nzuri ya kurudia kutwaa tuzo ya mchezaji bora kutoka msimu uliopita ambapo alitwaa na ingekuwa ni kwa mara ya pili mfululizo. Kwa bahati mbaya, jeraha lilimuweka nje kwa karibu miezi miwili na kuruhusu wengine kuchukua kasi.

Lakini raia huyo wa Norway bado anawindwa sana na tuzo nyingine ya mchezaji bora wa msimu huku akikaa kileleni kwenye mbio za Kiatu cha Dhahabu akiwa amefunga mabao 18 na asisti tano katika michezo 23 ya Ligi Kuu. 

Haaland alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu na mchezaji bora chipukizi katika kampeni msimu uliopita.

Kwa wakati huu, kila mtu anakosa uwezo wa kumuelezea fowadi huyo wa Manchester City. Huku City wakikimbia kuwania taji lao la nne mfululizo la Ligi Kuu, watamtegemea Haaland na mabao yake kuwafikisha mbali zaidi. 

#4. Ollie Watkins (Aston Villa)

Umekuwa msimu wa aina yake kwa Ollie Watkins na Aston Villa huku wakiendelea kupigania nafasi ya kuingia kwenye nafasi nne za juu za Ligi Kuu England. Villa chini ya kocha Emery Unai wameingia msimu huu wakiwa na ustadi wa juu, mpangilio na uchezaji bora, wakiongozwa na Watkins.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa anashika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu ya England akiwa amefunga mabao 16 na ana pasi 10 za mabao. Akiwa anaongoza kwenye mchango wa mabao 26 kwa jina lake kwenye ligi, Watkins amekuwa chanzo cha mabao ya Villa msimu huu.

Villa wameshindwa katika michezo ya hivi karibuni. Lakini tunapokaribia mwisho wa msimu, watategemea kiwango cha ufungaji mabao ili kuwaongoza kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

 #3. Declan Rice (Arsenal)

Rekodi ya kusajiliwa Arsenal ya pauni milioni 105 imekuwa yenye thamani ya kila senti moja hadi sasa. Baada ya kuyumba katika mechi 10 za mwisho za ligi msimu uliopita, Declan Rice amewapa 'Washikabunduki' uongozi unaohitajika na uimara wa ulinzi.

Kiungo huyo wa kati wa safu ya ulinzi hana kifani linapokuja suala la kukaba, akiwa amezui mara 35 katika mechi 28, ambayo ni ya sita kwenye ligi na ya juu zaidi kwa kiungo yeyote katika klabu sita bora. Ili kwenda sambamba na uwezo wake wa ulinzi, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amefanikiwa kufunga mabao sita ya msimu mmoja na kutoa pasi tano za mabao.

Rice amecheza katika kila mechi ya ligi msimu huu na ataendelea kufanya hivyo kwani Arsenal itakuwa ikitafuta taji lao la kwanza la ligi baada ya miaka 20. Iwapo Arsenal watalitwaa taji hilo Rice atakuwa mmoja wa washindani wa tuzo ya mchezaji bora wa msimu.

 #2. Phil Foden (Manchester City)

Ni wachache sana wanaoweza kubishana na Pep Guardiola wakati kocha wa Manchester City aliposema Phil Foden ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu England baada ya mabao yake mawili dhidi ya Manchester United. Nyota huyo amebarikiwa kuwa na kipaji cha ubunifu, ambaye anaonekana kuwa mchezaji kamili akiwa na umri wa miaka 23 pekee.

Ni bidhaa ya akademi ya Man City tayari ina msimu wake bora mbele ya goli akiwa amefunga mabao 11 katika michezo 28 ya ligi na asisti saba kwa jina lake.

Uchezaji wake katika miezi ya hivi karibuni umemsukuma hadi namba mbili katika viwango. Ikiwa ataendelea hivyo, atakuwa mchezaji wa kwanza wa England kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu tangu Jamie Vardy mnamo 2016.

 #1. Rodri (Manchester City)

Rodri ameendelea kuwa katika kiwango kizuri. Mchezaji wa tatu wa Manchester City katika orodha hii, lakini bila shaka ndiye aliye muhimu zaidi kwa timu hiyo - Rodrigo anatoa homchango wa hali ya juu na kuwa kiungo bora zaidi wa ulinzi duniani, achilia mbali Ligi Kuu England. Kiungo huyo wa ulinzi anaongoza ligi akiwa na pasi nyingi zaidi (2634) na miguso (2989).

Man City wanacheza kwa kasi anayocheza Rodri kwani mara nyingi inaonekana wanatatizika anapokosekana. Wakati Haaland, De Bruyne na Foden wakinyakua vichwa vyote vya habari, ni Rodri ndiye anayeichezesha timu nzima.

Raia huyo wa Hispania amekuwa na ufanisi katika nafasi ya tatu ya mwisho akiwa na mabao sita na asisti tano katika jumla ya mabao yake. Anaweza kutegemewa kila wakati na mara nyingi huja na bao katika mechi kali zaidi. Kwa vile wachezaji bora kama Haaland na Salah wamekosa mechi chache msimu huu, Rodri ana nafasi nyingi ya kubeba tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu.