Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, amewataka Watanzania kuendelea kuilinda, kuitunza na kuienzi amani, umoja na utulivu wa Taifa kwa vitendo.
Amesisitiza wananchi kutokubali kushawishiwa na watu wanaoishi nje ya nchi wasiolitakia mema Taifa, wanaotumia lugha ya uchochezi kama silaha ya kuvuruga mshikamano wa Watanzania.
Maulid alisema hayo jana, Februari 02 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kaselya, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne mkoani hapa kuelekea Maadhimisho ya Miaka 49 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maulid ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Singida, alisema kuwa Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani kutokana na mshikamano wa wananchi, hali inayopaswa kuendelezwa kwa gharama yoyote.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED