NI jambo la aina yake, hata ikirejewa katika tafakari ya kawaida tu, ikidodoswa kwa swali “Je, unaweza kujua umri wa mtu uliyekaa karibu naye kwa kunusa harufu ya mwili wake?
Mtu huyo anaweza kuwa hajajipuliza marashi, lakini unaweza kuujua umri wake kutokana na harufu ya mwili wake.
Bado kunatajwa, hakuna nadharia rasmi kuhusu hilo, lakini kuna utafiti unaothibitisha hayo kunusa ‘harufu’ ya mtu kubainisha umri wake.
Harufu ya mwili inatajwa kutofautiana kwa kila mtu, lakini hubadilika kadri anavyoendelea kuishi.
Ni mabadiliko ambayo mazingira anayoishi, bali hata mwelekeo wake kijamii na kimageuzi.
Wakati wa utotoni, inaelezwa kitaalamu, harufu ya mtoto huwa kidogo kutokana na tezi za jasho zisizo na shughuli nyingi, pia viumbe hai vidogo kwenye ngozi.
Hata hivyo, wazazi wengine wanatajwa wanaweza kugundua harufu ya watoto wao zaidi, kuliko watoto wa wenzao.
Harufu hiyo inatajwa kuunda uhusiano mzuri wa kihisia na kawaida, kati ya wazazi na watoto wao.
Pia, husaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa wazazi, huku ikijenga hisia za furaha na upendo kwa mtoto.
Hapo kuna harufu maalumu inayotokana na watoto wanaokuwa, ikiwavutia zaidi.
Hata hivyo, inatajwa kinamama wanaosumbuliwa na hali ngumu kiafya baada ya kujifungua, kuna wakati hawawezi kunusa harufu ya mwili ya watoto wao.
KUNUKIA MTOTO
Wakati wa umri wa kubalehe, harufu ya mwili ya mama hubadilika kila wakati.
Ni mabadiliko hayo yanayosababishwa na uzalishaji wa homoni za kijinsia, ambazo husisimua tezi za jasho na tezi za mafuta kwenye ngozi. Tezi nyingi za jasho huzalisha maji na chumvi.
Wakati tezi ziitwazo ‘Aprokrini’ huzalisha protini na mvuke unaohusiana na mafuta. Tezi hizo huzalisha harufu mbalimbali, ambazo ni za kipekee kwa kila mtu.
Pia, kinachoitwa ‘Lipidi’ na ‘Sebum’ ni kemikali ya mafuta inayolainisha nywele, ngozi na ngozi ya kichwa hutolewa kutoka kwa tezi hizo. Hata hivyo, ikichanganyika na bakteria, harufu ya miili ya binadamu huwa vibaya.
Hiyo ni sambamba na jasho la vijana, pamoja na harufu za miili yao, hubadilika na kutoa harufu mbaya.
Wanapofika umri wa kubalehe na kuingia utu uzima, harufu yao ya mwili inapungua na hivyo kupunguza uwezo wa wazazi kutambua watoto wao kwa harufu.
Kwa ujumla, kila mtu ana harufu maalum ya mwili, lakini inabadilika kadiri anavyokuwa.
UTAJUAJE HARUFU YAKO?
Kuna swali, mtu atajuaje harufu yake? Hapo kuna maelezo kwamba utoaji mafuta katika tezi hizo, huongezeka wakati wa hatua ya kubalehe.
Ingawa nguvu zake hupungua mtu anapozeeka, kila mtu tayari anakuwa na harufu maalumu mwilini.
Hii inatajwa, kutegemea mambo mengi kama vile lishe, msongo wa mawazo, homoni, pia viumbe hai vya ngozi yake.
Uwezo wa mtu kunusa unatajwa kuwa mzuri sana katika kubaini habari kujihusu, hasa kiwa gizani au mazingira yaliyo na kelele, au wakati ambao ni vigumu kuona au kusikia kwa urahisi.
Harufu ya mwili husaidia katika kuchagua wapenzi, kutambua jamaa, au kutofautisha jinsia.
HALI YA UZEENI
Mtu anapozeeka kitaalamu anaelezwa, ngozi yake hupoteza ubora na vimelea ‘Kalojeni’. Hiyo inatajwa kupunguza shughuli za tezi za jasho na mafuta yake na kutokana na upungufu huo, inakuwa vigumu kwa wazee kudumisha joto la mwili.
Kuhusu tezi ziitwazo ‘Sebasi’, utoaji wao hupungua kadri mtu anavyozeeka; muundo wao pia hubadilika.
Ni hali inayosababisha kupungua kwa viwango vya Vitamini E au ‘Squalene’ ambavyo huzuia uzalishaji zaidi wa Oksijeni mwilini.
Ujumla wake unasababisha kuwapo harufu kwa wazee, ambayo Wajapani huita 'Kerisho'.
Hivyo, baada ya mtu kuwa na umri wa miaka 40, kazi ya baadhi ya tindikali za mafuta kwenye ngozi kama vile ‘Omega 7’ na ‘Palmioleic’ hubadilika. Hilo hubadilisha harufu ya mwili wa binadamu kwa ujumla.
*Kwa mujibu wa BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED