MGUNDUZI LULU HUNT; Mtaalamu lishe bora

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:45 AM Jan 02 2025
Lulu Hunt
Picha: Mtandao
Lulu Hunt

IDADI ya kalori huonekana kwenye lebo nyingi za vyakula na vinywaji vilivyopakuliwa na hata kwenye menyu za baadhi ya migahawa. Taarifa hizo zinapatikana kwingi.

Dunia iliyopiga hatua kiteknolojia, mtu anaweza kujua hatua za kutembea, akachoma kalori zake kila siku kwa kutazama kipimo kwenye simu yake.

Pia, kwenye ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo, pia kunatajwa kuwapo vielelezo vya kalori.

Msingi wake kalori, ni neno la Kilatini “calor” linalomaanisha ‘joto.’ Liligunduliwa kwa mara ya kwanza na mtaalamu Mfaransa wa Kemia na Fizikia, Nicolas Clément katika miaka 1820.

Kalori ilikuwa kipimo cha joto kinachoweza kubadilishwa kuwa nishati, na kilitumika kupima kiasi cha mvuke kuendesha injini za mitambo.

Suala la kuhesabu kalori ilikuwa jambo geni karne moja iliyopita. Nafasi yake kuwa kipimo cha lishe, ilianza kutumika mwishoni mwa Karne ya 19.

Hapo ndipo miaka 1920, mtaalamu Lulu Hunt Peters, daktari wa Kinarekani, mhitimu wa Chuo Kikuu cha California, akafanya mageuzi kuja na mahesabu ya kalori.

Ghafla akawa wa kipekee, maana wakati huo wanawake walikuwa chini ya asilimia tano ya wanafunzi wanaosomea udaktari nchini Marekani.

Ingawa sasa kalori zinajulikana kwa kuhesabu, tafiti zinaonyesha kwamba karibu asilimia 80 ya watu wanaopunguza uzito mkubwa kwa kupunguza ulaji wa kalori, wanarudi tena kwenye uzito wao wa awali.

KIPIMO CHA CHAKULA

Maana ya leo ya kalori ya sasa (joto linalohitajika kuinua kilo moja ya maji kutoka nyuzi joto 0 hadi 1° Celsius) iliingia kwenye uwanja wa lishe ya binadamu, kutokana na kazi ya mtaalamu wa kemia, Mmarekani, Wilbur O. Atwater.

Atwater alichukua likizo ya mwaka mmoja kwenda Ujerumani, alikojifunza kutumia kipima joto kinachoitwa Kalorimeter, kifaa kinachotumika kupima kiasi cha joto kinachotolewa au kupokewa na miili.

Wakulima wa Kijerumani walikitumia kuzalisha chakula bora kwa mifugo yao.

“Aliporejea kwenye maabara yake huko Connecticut, Atwater alijaribu kurudia mchakato huu, si kwa ajili ya lishe ya mifugo, bali kwa ajili ya chakula cha binadamu,” anaeleza Profesa Giles Yeo, mtaalamu wa Niurolojia (neuroendocrinology) katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza.

Hapo akaanza kuchapisha majarida yenye maelezo ya kina kuhusu kalori o katika vyakula, kiasi kinatoka kwenye lishe za; protini, mafuta na kabohaidreti.

Kwa sasa inaonekana jambo lililozoeleka kufahamu tufaha lina kalori kidogo ukilinganisha na donati haikuwa imejulikana miaka 100 iliyopita

“Kanuni maarufu inayofundishwa shuleni (kalori 4 kwa gram 1 ya protini, kalori 4 kwa gram 1 ya kabohaidreti, na kalori 9 kwa gram 1 ya mafuta), anasema mtaalamu Yeo,

 ZAMA UTAPIAMLO

Wakati utapiamlo ulikuwa tatizo, taarifa hizo zilikuwa muhimu kusaidia jamii maskini kula vizuri kwa rasilimali chache walizo nazo.

“Awali, watu walijali zaidi ni kalori ngapi wataweza kupata kwa bei rahisi,” anasema Helen Zoe Veit, mtaalamu wa historia ya chakula katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan, Marekani.

“Hata waajiri wengine walitumia kalori kuthibitisha malipo ya chini, wakisema, ‘kulingana na hesabu ya kalori, unapaswa kuwa na uwezo wa kununua chakula cha kutosha kwa kile tunachokulipa,’” anasema pia mtaalamu huyu wa historia ya chakula.

MABADILIKO KIJAMII

Mwanzoni mwa karne ya 20, wakati upatikanaji chakula uliongezeka na maendeleo ya teknolojia mpya za kuhifadhi na kusafirisha chakula, idadi ya watu, hasa nchini Marekani ilianza kuongezeka. 

Akiwa ameelewa kazi za Atwater kupitia taaluma yake, daktari huyo alikuja na wazo la kutumia zana zilezil, kuhesabu kalori, katika kampeni za kupunguza kilo alizoziona tatizo.

Akatumia mantiki ya kimaandishi (kula kidogo kuliko unavyotumia), Lulu, ambaye wakati huo alikuwa na uzito wa karibu kilo 90, alifanikiwa kupunguza karibu 30.

Akafurahishwa na matokeo hayo na  akaanza kuandika kila mara matokeo yake kwenye safu ya makala katika magazeti ya wakati huo, akielezea mbinu yake yaa kupunguza, hatimaye akaandika kitabu chake.

Hapo mitindo pia ilibadilika, kulingana na dhana mpya ya uzuri inayohimiza mwili wenye umbo uliochongeka.

Mtindo mwingine uliipatia umaarufu wakati huo, ni kuwa kama vile mkanda wa kiunoni ulioanza kupitwa na wakati.

Mafanikio ya Lulu katika kubadilisha mwili wake kuwa unaohamasisha, kitabu chake kikawavutia hasa wanawake (weupe na tabaka la kati).

“Ni kitabu kilichoandikwa vizuri,” anasema Profesa Yeo, ingawa leo maoni yake yangetafsiriwa kama ubaguzi dhidi ya watu wanene, maandiko yake ni ya kufurahisha na ya kuvutia,” anasema.

Mwamdishi mwenyewe alikuwa na uzito wa ziada, hivyo maoni yake wakati huo yalionekana ya kujikosoa, badala ya kumshtumu mtu kuwa “mnene kupita kiasi”.

UZITO NA AFYA

Lakini kitabu hicho kilikuwa na athari kubwa kwa sababu kuna wakati, maono mapya ya mwili yalikuwa yakijitokeza, pia kwa sababu uhusiano kati ya mafuta ya ziada mwilini na afya ulianza kugunduliwa.

“Katika miaka ya 1910, ushahidi mpya ulionyesha kuwa uzito kupita kiasi unaweza kuwa na madhara,” anasema Veit.

“Tafiti zilizofanywa na makampuni ya bima, kwa mfano, zilionyesha kuwa kadri watu wanavyokuwa na uzito mkubwa baada ya umri wa miaka 35, ndivyo walivyokuwa na uwezekano mkubwa wa kufariki,” anafafanua

Ingawa mapendekezo ya Peter yaliangazia kalori 22, akielewa kuwa unapaswa kula kwa kiwango hitajika na kula lishe bora, lakini hakukataza kabohaidreti, nyama na maziwa. 

Mtaalamu Profesda Yeo, anaelezea kwamba, mti akilinganisha miiko kupunguza unene kupita kiasi, kama vile matumizi ya aina fulani za dawa za kulevya; uvutaji sigara na matumizi ya mipira.

Mkakati wa mtaalamu Peter, haukuwa na ishara kuwa haufuati maagizo ya kiafya.

MATUMIZI YA KALORI 

Kuzingatia habari mpya kuhusu lishe, muundo wa chakula, mwili wa binadamu unavyofanya kazi, tunafahamu njia ya bora ya kuhesabu kalori, huku tykudumisha lishe bora au hata kupoteza uzito kwa njia endelevu.

Bado, hamu ya kuhesabu haijaisha kabisa katika mtindo na wengi wanaamini kuwa, mawazo hayo yanachangia kukabili shida iliyoko katika jamii ya unene kupita kiasi.

Ingawa kalori hazina maana ya moja kwa moja afya ya mtu, lakini bado ina matokeo katika maisha, Profesa Yeo, akiwa na ufafanuzi: "Ni njia rahisi ya  kufanya maamuzi, lakini inamaanisha kuzingatia jambo lisilofaa."

Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa.