VIONGOZI wa dini na wakazi wa Mkoa wa Tanga wameunga na Mkuu wa mkoa huo Dk. Batlida Buriani kufanya maombi ya kuliombea Taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu na viongozi wengine ili nchi iweze kudumu katika amani na kutulinda na mabalaa.
Maombi hayo yamefanyika leo katika viwanja vya urithi kama sehemu tamasha la Tanga urithi festival ambalo limejikita katika kutangaza fursa za utalii, tamaduni za watu wa Tanga sambamba na kuwarithisha vijana tamaduni za watu wa pwani.
Akiongea na wananchi wa Tanga Mwenyekiti wa kamati ya amani Mkoa wa Tanga Shekhe Jumaa Luwuchu alisema kuwa Dua hiyo ni kumshukuru mungu kwa ajili ya kuwapatia neema ya viongozi Mahiri na waadilifu nchini Tanzania.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk. Batlida Buriani amesema kuwa mkoa wa Tanga umeweza kufanyiwa maendeleo makubwa na serikali kwenye sekta mbalimbali kama vile elimu, uchumi, afya na hata biashara.
"Tunamshukuru Rais Samia kwa maboresho makubwa ya Miradi ya kimkakati ambayo imeweza kusaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi" amesema RC Buriani.
Hivyo uwepo wa Dua hii ni sehemu ya kumshukuru mungu lakini na kuendelea kumuomba aweze Kudumisha Umoja na amani katika mkoa wetu sambamba na wananchi wetu kwa ujumla.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED