WATOTO wa tatu wa familia mmoja, wamepoteza maisha, baada ya kufa maji wakati wakigolea kwenye lambo la kunywesha maji mifugo lililoko Kijijii cha Ngaritati, Kata ya Makiwaru, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata hiyo, Ezekiel Lukumayi, amesema watoto hao wamekufa maji jana Junuari 2 mwaka huu.
Amesema kabla ya umauti kuwafika, watoto hao walikuwa wameenda katika eneo hilo kwa ajili ya kufua nguo na kuoga.
"Ni kweli watoto hao wamefariki dunia kwenye lambo hilo la Ngaritati, wakati wakiogelea. Mmoja wa waliopoteza maisha ana umri wa miaka tisa. Huyo ni mwanafunzi wa darasa la nne wa Shule ya Msingi Ngaritati na hao wawili wana umri wa miaka sita, wanasoma chekechea (darasa la awali)."
Kwa mujibu wa Diwani Lukumayi, kati ya waliokufa maji, watoto wawili ni wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lambo, na mmoja ni wadungu yake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED