52 wafanyiwa upasuaji wa macho

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 01:11 PM Dec 30 2024
Wataalam wa macho upasuaji
Picha: MNH
Wataalam wa macho upasuaji

WATU 52 kati ya 405 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa ya macho, ikiwamo kuondoa mtoto wa jicho, huku mmoja akipatiwa rufani ya kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Joseph Peramiho, kwenye kambi ya siku nne, iliyoandaliwa na MNH pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma, kuanzia Desemba 26 hadi 29, 2024.

Mtaalam wa macho akitoa huduma
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Dk. Geofrey Kihaule, alisema kwamba wananchi 27 kati ya 405, wamepatiwa miwani kutokana na changamoto za uoni hafifu, huku wengine wakipatiwa matibabu ya kawaida ya macho. 

Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka MNH, Dk. Joachim Kilemile, alisema kuwa huduma zilizotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya macho, utoaji wa miwani na dawa kwa wenye matatizo ya macho. 

Mtaalam wa macho akitoa huduma