Tanzania yashika namba 9 miundombinu bora ya barabara

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 06:25 PM Nov 04 2024
Tanzania yashika namba 9  miundombinu bora  ya barabara
Picha: Mtandao
Tanzania yashika namba 9 miundombinu bora ya barabara

Tanzania imetajwa kuwa kati ya mataifa 10 bora barani Afrika ambayo yana miundombinu bora ya barabara.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mtandao wa Statista ikichapishwa na businessinsider, Tanzania kati ya nchi 10 bora ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 4.41.

Taarifa hizi zinakuja ikiwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kuanzia mijini hadi vijijini.

Uwekezaji huo unalenga kuwarahisishia wananchi, kufanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji kwa urahisi ili kuharakisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

1