Aliyechoma maiti ya mke wake hakuwa na akili timamu

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 05:07 PM Nov 04 2024
Mfanyabiashara Khamis Luwonga, akiwa kizimbani.
Picha:Grace Gurisha.
Mfanyabiashara Khamis Luwonga, akiwa kizimbani.

RIPOTI kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili, Mirembe imeeleza kuwa mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa wakati anafanya tukio hilo la mauji alikuwa ana shida ya akili.

Taarifa hiyo, imetolewa leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwasiti Athuman mbele ya Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji.

Wakili Athuman amedai kuwa katika kikao cha mwisho Mahakama ili ekelekeza mshtakiwa apelekwe kwenye Hospitali ya Afya ya akili kuangalia akili yake wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana akili timamu au la.

Amedai ripoti ya kitababu ya hospitali hiyo ya Septemba 26, 2024 katika ukurasa wake watatu inaeleza kuwa baada ya mshtakiwa kufanyiwa uchunguzi wakitaalamu walioona anaugonjwa wa kifafa ambapo alipewa dawa. 

Pia, amedai  kuwa ilionekana mshtakiwa huyo wakati anafanya tukio hilo alikuwa ana shida ya akili, kutokana na ushahidi huo ni wa upande wa utetezi wapo tayari kuendelea na usikilizwaji na wana mashahidi wawili.

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.