Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa baa maarufu jijini Dodoma ya ‘Chako ni Chako’, Honorath Makoi unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Kibosho, mkoani Kilimanjaro Alhamisi ya Novemba 07, 2024.
Makoi (35) amefariki dunia alfajiri ya saa 10 jana Jumapili Novemba 03, 2024 Dodoma baada gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kugonga mti wakati akirejea nyumbani kwake Swaswa jijini humo.
Inaelezwa kuwa Maiko amefikwa na mauti akiwa ameshamvisha pete mchumba wake na kilichokuwa kikisubiriwa ni kufunga ndoa.
Leo Novemba 04, 2024 Msemaji wa familia ya marehemu,Hendry Sindato amesema mipango ya mazishi ya Makao inafanyika nyumbani kwake Swaswa na mwili wake unatarajiwa kuagwa Jumatano ya wiki hii (Novemba 06) na kisha kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Kibosho kwa maziko.
“Marehemu alikuwa bado hajaoa, ila alikuwa na mchumba ambaye sisi kama familia tulikuwa tunamtambua kwa sababu tayari alishamvisha pete, ilikuwa bado tu kuoana na walikuwa hawajapata mtoto …ila kama alikuwa na watoto huko nje tutajua baadaye,” amesema Sindato.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED