WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kwenye Maonesho ya yanayofanyika pembezoni mwa mkutano wa Mameneja Rasilimali Watu Afrika, jijini Arusha, Novemba 4, 2024.
Akiwa katika banda hilo, Majaliwa alipokelewa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, PSSSF, Paul Kijazi, ambaye alimueleza jinsi mfuko huo ulivyotehamisha huduma zake, kutoka matumizi ya karatasi hadi yale ya kidigitali.
“Utakumbuka mwezi Agosti, 2022, wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa PSSSF, ulituzindulia Huduma za wanachama kidijitali, huduma ambayo imerahisisha utoaji wa huduma zetu.” amesema Kijazi.
Akifafanua amesema, kupitia simu janja, mwanachama anaweza kutuma madai mbalimbali, lakini pia anaweza kuona mwenendo wa michango yake, kuuliza maswali na kujibiwa, lakini wastaafu nao wanaweza kujihakiki.
Kwa sehemu kubwa huduma za PSSSF Kidigitali imepunguza gharama, kuondoa usumbufu na kuleta uwazi, alisema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED