Tigo, TRC waungana wiki huduma kwa Wateja

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 03:47 PM Oct 08 2024
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Jerome Albou (kulia) akimpa zawadi mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kwa miaka 30 ndani ya behewa la SGR leo.
PICHA: FAUSTINE FELICIANE
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Jerome Albou (kulia) akimpa zawadi mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kwa miaka 30 ndani ya behewa la SGR leo.

WAKATI wakiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja na kumbukumbu miaka 30 tangu kuanza kutoa huduma Tanzania, Kampuni ya simu ya Tigo imesafiri na baadhi ya wateja wake waliodumu kwa miaka yote kwenye kampuni hiyo kuelekea Dodoma na usafiri wa reli ya SGR.

Akizungumza mara baada ya kufika Dodoma, Afisa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo, Isaack Nchunda, amesema maadhimisho hayo yameenda pamoja na kuanzishwa kwa ushirikiano kati kampuni hiyo kupitia Tigopesa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambapo sasa wateja wanaweza kununua tiketi kupitia huduma hiyo.
 
"Kampuni ya Tigo ndiyo mtandao mkubwa wenye kasi zaidi Tanzania toka mwaka 1994 mpaka sasa ambapo ni historia ambayo imechangia maendeleo ya wateja wake binafsi na kufikia mafanikio mbalimbali," amesema Nchunda.

Huduma kwa wateja mwaka huu imeenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘Above & Beyond ‘ ambayo inathibitisha kwamba Tigo wako sako kwa bako na wateja wake.