WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali inatarajia kujenga Bwawa la Mkomazi kwa ajili ya umwagiliaji linalotarajia kunufaisha wananchi zaidi ya 20,000 kutoka katika Kata zaidi ya saba na vijiji zaidi ya 28 mkoani Tanga.
Bashe amesema ujenzi wa Bwawa hilo ilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, hivyo Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuitimiza kwa kutenga fedha za ujenzi wake.
Bashe amesema ujenzi wa Bwawa hilo ilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, hivyo Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuitimiza kwa kutenga fedha za ujenzi wake.
“Wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa Bwawa la Mkomazi hatimaye mtashuhudia ndoto ya Hayati Julius Nyerere ya kutaka kujenga bwawa hilo la umwagiliaji, ambayo sasa inakwenda kutimizwa na Rais Samia,”alisema Bashe.
Amesema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa mabomba mawili yenye urefu wa kilomita 16 na 29 ambayo yatakuwa yanasafirisha maji pande tofauti pamoja na ujenzi wa mifereji mikuu, mifereji ya matupio, ujenzi wa ghala, kituo cha zana za kilimo, mashine ya kukoboa mpunga, barabara za mashamba na za kusafirishia mavuno.
Kadhalika, Bashe ameielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kuhakikissha wafugaji wanatengewa eneo la kunyweshea mifugo na kuzungushia uzio wa umeme bwawa hilo la Mkoamazi ili kulinda miundombinu yake..
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED