Waziri Chana awataka watumishi kuwa wabunifu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:07 PM Dec 21 2024
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk. Pindi Chana.
Picha: MWANDISHI WETU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk. Pindi Chana.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk. Pindi Chana amewaasa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake kutekeleza majukumu yao kwa ubunifu katika kuendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii.

Ameyasema hayo leo Desemba 21,2024 katika Mkutano wa 32 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Utalii Ngorongoro jijini Arusha.

"Lazima tufanye kazi za Watanzania ambao wametupa dhamana kwa ari na ubunifu wa hali ya juu" Chana amesisitiza.

Aidha, ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaendelea kusikiliza madai na changamoto za Utumishi na kuzitatua.

Amewataka kutumia fursa ya baraza hilo kujadili hoja za kiutumishi, mustakabali ya hali za Utumishi na utekelezaji wa malengo ya Sekta ya Maliasili na Utalii.