NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, amewahimiza wananchi kuchangamkia uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuinua vipato vyao.
Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala, jijini Dar es Salaam, ameyasema hayo leo Desemba 20, 2024, mara baada ya wasilisho la Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Mbaruku Magawa, kuelezea mafanikio ya PSSSF katika miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan, kwenye semina ya viongozi wa Kata na Mitaa wa Wilaya ya Ilala.
“Tumepata mafunzo makubwa na mazuri, niwaase ndugu zangu, kuna fursa nyingi za uwekezaji PSSSF, changamkieni fursa hizo, hata kama wewe ni kijana bado hujastaafu, unaweza kuwekeza kupitia mfuko na ukajikuta unaongeza kipato chako.” amesema Zungu.
Akitoa wasilisho la PSSSF kwenye semina hiyo, Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Mbaruku Magawa amesema, yapo mafanikio mengi yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani.
“Kupitia uwekezaji tuliofanya kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda, jumla ya watu elfu 34,000 wamefaidika, kupata ajira za moja kwa mmoja na zisizo za moja kwa moja,” amefafanua Magawa
Aidha, mafanikio mengine Magawa mesema, ni PSSSF kuanza kutekelea maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye alisikia kilio cha wastaafu kutaka nyongeza ya pensheni.
“Kuanzia mwezi ujao wa Januari, 2025, Wastaafu wanaopokea pensheni kutoka PSSSF wataanza kupokea nyongeza ya asilimia
“Wastaafu wote awameongezewa asilimia 2% kwenye pensheni yao, lakini pia serikali imeelekeza endapo mstaafu atafariki, Mfuko utatoa ubani wa mazishi, shilingi laki 500,000, jambo la tatu kuanzia januari mstaafu yoyote akifariki, wategemezi wake watalipwa mkupuo wa pensheni ya miezi 36, na haya yote yamefanyika chini ya serikali ya awamu ya sita.” amefafanua.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED