Serikali kuboresha Bandari ya Tanga mapato kuongezeka mara nne

By Hamida Kamchalla , Nipashe
Published at 07:47 PM Dec 20 2024
Bandari ya Tanga.
Picha: Mpigapicha Wetu
Bandari ya Tanga.

SERIKALI ina mpango wa kuendelea kufanya maboresho zaidi katika Bandari ya Tanga jambo ambalo llinatarajiwa kuaongeza mapato zaidi kutoka bil 100 za sasa na kufikia kiasi cha shilingi Bilioni 400 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa alipotembelea bandari hiyo na kusema kuwa serikali itaongeza ujenzzi wa gati nyingine yenye urefu wa mita 350 zaidi ambazo zitakamilisha mita 750 pamoja na mita 400 za uboreshwaji wa awali.

Waziri Mbalawa amefafanua kwamba maboresho hayo yanafanyika katika bandari zote nchini ambapo wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) wanatekeleza agizo la Rais.

"Kila mkoa unapoenda ambao kuna bandari kunafanyiwa marekebisho, kubwa ni sisi wajibu wetu mkubwa ni kuendelea kuchapa kazi na tupeleke ujumbe kwamba uwekezaji huu ni sahihi kwa manufaa ya wananchi wa Mkoa wa Tanga lakini pia na nchi kwa ujumla" amesema.

Amebainisha kwamba awali kabla ya maboresho hayo hata pato la Mkoa huo lilikuwa chini ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana lakini maisha yamekuwa tofauti kwasasa ambapo pato limeongezeka kwa kiasi kikubwa