Diwani Shinyanga afariki dunia

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 01:59 PM Oct 08 2024
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Sonya Mhela.
Picha: Marco Maduhu
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Sonya Mhela.

DIWANI wa Kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Sonya Mhela amefariki dunia, akipatiwa matibabu Bugando Jijini Mwanza.

Taarifa za msiba huo zilitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje ambaye amesema wiki iliyopita Sonya alipata ajali ya pikipiki akavunjika mguu. 

Amesema baada ya kupata matibabu ya awali alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, lakini wakati akiendelea na matibabu hali yake ilibadilika na kufariki dunia.

Mazishi ya diwani huyo yamefanyika jana Oktoba 7,2024 nyumbani kwake Itwangi.