Kapinga kunadi fursa uwekezaji mafuta, Gesi Asilia na Nishati mbadala Afrika Kusini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:15 PM Oct 08 2024
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga.
Picha:Mpigapicha Wetu
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameshiriki Jukwa la Mawaziri (Ministerial Symposium) nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemu Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week) linalofanyika Jijini Cape Town.

Jukwaa hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dk. James Mataragio, Kamishina wa Petroli na Gesi, Goodluck Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mha. Charles Sangweni.

Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.

Kongamano hilo litamalizika Oktoba,10, 2024 nchini humo.