Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk. James Andilile, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhudumia wateja wake kwa kuzingatia Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa EWURA ni maafikiano kati ya EWURA na wateja wake, ambao ni wadau wakuu katika shughuli za udhibiti na umeorodhesha wadau wakuu wa EWURA, huduma zitolewazo pia viwango vya ubora wa utoaji huduma ambavyo wateja wanatarajia.
Akizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja kwenye Ofisi hiyo, Dk.Andilile amesema “EWURA hatuna bidhaa tunayozalisha, hivyo kama mtu anataka kutathmini utendaji wetu wa kazi ataangalia zaidi namna ambavyo tunatoa huduma kwa wateja.”
Dk. Andilile amewataka Wafanyakazi wa EWURA kuboresha utendaji kazi na ushirikiano ili kufikia malengo ya taasisi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED