Mama yake Whitney Houston afariki dunia

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 06:23 PM Oct 08 2024
CISSY Houston (91)
Picha: Mtandao
CISSY Houston (91)

CISSY Houston (91), aliyekuwa mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili na mamake Whitney Houston, amefariki dunia. Familia yake imesema katika taarifa.

Houston, ni mwimbaji aliyeshinda Tuzo ya Grammy mara mbili, alimrithisha mwanaye Whitney uimbaji, akitamba duniani kote.

Amefariki Jumatatu, nyumbani kwake New Jersey alipokuwa katika huduma ya wagonjwa wa Alzheimer, binti-mkwe wake Pat Houston amesema.

“Mioyo yetu imejaa uchungu na huzuni. Tumempoteza mama wa familia yetu,” alisema, akiongeza kuwa mama mkwe wake alikuwa mtu hodari na imara katika maisha ya familia hiyo.

Houston, alifurahia kazi ya uimbaji yenye mafanikio ya miongo kadhaa, aliigiza pamoja na wasanii maarufu kama Elvis Presley na Elvis Presley

BBC