MAHAKAMA imemwachia huru mwanamuziki maarufu wa hip hop nchini Marekani, Drake, baada ya kumuona hana hatia katika kesi inayohusu tamasha la Astroworld 2021 lililofanyika Houston ambalo lilisababisha watu 10 kufa kwa kukosa hewa.
Katika tamasha hilo, Drake alikuwa mgeni maalumu wa msanii mwenzake Travis Scott, ambaye aliandaa onyesho hilo.
Mwishoni mwa tamasha hilo lililofanyika Novemba 5, umati wa watu ulipoongezeka katika eneo la tukio na kusababisha hali ya mkanyagano uliofanya wengi kuathiriwa kwa kukosa hewa,
Ilidaiwa mamlaka ya eneo hilo na waandaaji wa tamasha walijaribu kukatisha tamasha hilo, lakini haikusaidia kwani maafa yalizidi na kufanya watu 10 kufa papo hapo kwa kukosa hewa.
Walishtakiwa ikiwamo Drake na Scott, walimwomba Jaji wa mahakama hiyo ya Wilaya, Kristen Hawkins kufuta kesi dhidi yao na ombi hili lilikubaliwa kwa upande wa Drake na kutakiwa kuondoka mahakamani hapo.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED