Waeleza umuhimu wa mafunzo JKT

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:20 PM Oct 07 2024
 Waeleza umuhimu wa mafunzo JKT
Picha:Mpigapicha Wetu
Waeleza umuhimu wa mafunzo JKT

WANUFAIKA wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Operesheni Kambarage iliyofanyika Mwaka 1990 hadi 1991 katika kikosi 834 KJ Makutopora wameeleza umuhimu wa mafunzo hayo na namna yalivyowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uzalendo kwa maendeleo ya Taifa.

Mmoja wa viongozi wa kikundi hicho,  Vivian Komu amesema ni miaka 33 iliyopita tangu wamepata mafunzo hayo ambayo yamekuwa na manufaa  kwenye maisha yao na taifa.

"Hadi leo tunakutana hapa kila mmoja anamajukumu yake na ukweli ni kwamba nidhamu, uzalendo na ukakamavu wetu ni matokeo ya kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, "amesema Komu

Naye, Frida Marco amesema Taifa lipo salama kwa sababu ya kuwa na vijana wengi wanaopitia Jeshini, hivyo wazazi wasiwafiche watoto pindi wanapotakiwa kujiunga na Jeshi. 

" Wazazi waacheni watoto wajiunge na JKT kwa maslahi ya Taifa kwani mtoto akipata mafunzo ya Jeshi huwezi kusikia anajiunga na vikundi viovu, migomo ama maandamano yasiyokuwa na maana,kazi yake popote atakapokuwepo atakuwa anaweka maslahi ya Taifa mbele kutokana na Uzalendo na nidhamu aliyefundishwa kutoka Jeshini, " ameeleza Frida

Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi 834 KJ Makutopora, Kanali Festo Mbanga amewahamasisha watanzania kuwapeleka watoto kujiunga na JKT ili wapate  mafunzo yatakayowajengea uzalendo, ujasiriamali na ukakamavu. 

3