MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu umeanza kukabidhi Ilani ya Uchaguzi pendekezwa ya mwaka 2024-29 iliyoandaliwa na Asasi za kiraia zisizo za kiserikali katika vyama vya siasa vilivyokuwa vya kudumu vya siasa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema lengo ni kukabidhi ilani hizo ni kuimarisha usawa katika nyanja zote za huduma za kijamii, kimaendeleo, kiuchumi, demokrasi, usawa wa kijinsia, haki za makundi maalum walemavu na nyingine nying ambazo zimeanishwa katika ilani hiyo.
Amesema Ilani hiyo watawasilisha kwa vyama vyote vya kudumu vitakavyoingia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao 2025 wafuate Ilani pendekezwa kuwaongoza aina ya viongozi wanaowahitaji kupelekea mbele taifa la kwa kauli mbiu isemayo “Tanzania Tuitakayo” ambayo imeanisha viongozi wawe wa aina gani ikiwemo kuwa watetezi wa haki za binadamu.
"Wawe tayari kuleta Taifa pamoja, utulivu, kuvumiliana, kukosolewa, wenye kupiga vita rushwa, kujenga maswala ya utawala bora, asiyekubali kupitisha kupitisha sera ambazo sheria inakwenda kumuumiza mtanzania wa kundi lolote pamoja na awe mwenye kusimamia na kulinda rasilimali za nchi" amesema
Ameanisha Ilani hiyo imeandaliwa na Asasi za kiraisa zipatazo 300 ambapo kwa pamoja kipaumbele kikubwa namba moja ni kuhitaji Katiba Mpya hiyo ni ajenda ya msingi ili kupata uongozi.
Amesema wanataka viongozi wanaotafuta ridhaa na kuheshimu michakato yote ya kidemokrasia pamoja na kuheshimu Tunu za kitaifa ibara ya tisa imezungumza baadhi ya sifa ili tuwe na taifa endelevu na linasonga mbele kimaendeleo lazima kuwe na Tunu kama umoja, undugu, amani na utulivu, uadilifu, uwazi na uwajibikaji.
Kwa upande wake Doroth Semu Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara Chama cha ACT Wazalendo amesema wako tayari kuboresha ilani yao kwa kupitia ilani hiyo kwania ACT wanatamani kupata ilani ambayo inagusa na itaakisi uboresha na kugusa maisha ya wananchi wake wakiwemo wanyonge.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED