Aggy Simba ataka kusikilizwa sakata la kufungiwa kwake

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 01:52 PM Jul 22 2024
MWANACHAMA wa Klabu ya Simba Agnes Malkiad maarufu Aggy Simba.
Picha: Mtandao
MWANACHAMA wa Klabu ya Simba Agnes Malkiad maarufu Aggy Simba.

MWANACHAMA wa Klabu ya Simba Agnes Malkiad maarufu Aggy Simba, amelalamikia kitendo cha Sekretarieti ya Klabu hiyo kumfungia kujihusisha na masuala yanohusu klabu hiyo akitaka afikishwe katika kamati ya maadili kwaajili ya kuwasilisha utetezi wake.

Akizungumza na Nipashe Aggy amesema barua aliyopewa na sekretariet hiyo inasema amefungiwa kwa kosa la kuitisha mkutano kinyume cha taratibu na kuchochea migogoro ndani ya klabu jambo ambalo anadai siyo kweli.

“Ninakosa haki kama mwanachama wa Simba kwasababu barua inasema tutaitwa kwenye kamati ya maadili na hatujaitwa mpaka sasa ili nikasomewe mashtaka yangu na mimi niweze kusikilizwa.

“Siruhusiwi kujishughulisha na masuala ya klabu kama yapi? ninakosa haki ya kuwa huru. Kurushwa katika mitandao ya kijamii ya Klabu ya Simba kwamba nimefanya hayo mambo ni kulichafua jina langu” amelalamika 
Amesema barua inaeleza ataitwa katika kamati ya maadili lakini mpaka sasa bado hajaitwa na hajui nini kinakwamisha kupata haki yake.

Aggy, ambaye mbali na kuwa mwanachama wa simba pia ni mshabiki kindakindaki wa timu hiyo anashahuku ya kurejea kuendeela kuisapoti timu yake huku akisifu kitendo Mohamed Dewji Maarufu ‘Mo’ kurejea katika nafasi ya Uenyekiti wa Bodi na kueleza kitendo hicho kitaipatia timu hiyo matokeo chanya katika msimu ujao.