Kula parachichi, ujue unavuna mambo haya...

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:18 AM Oct 10 2024
Parachichi.
Picha: Mtandao
Parachichi.

UMAARUFU wa parachichi, unatajwa ni kutokana na umbile lake nyororo, laini na ladha isiyo ya kawaida. Parachichi ni tunda lililoko katika kundi la familia ya mdalasini. Kuna aina kadhaa ya parachichi, kuanzia ukubwa, rangi na muundo.

Yote yanakuwa na asili kuendana na hali ya hewa ya kitropiki na yanapovunwa, ni nyororo na laini kama siagi, hata kuwa maarufu sana katika kila kitu kuanzia kwenye kuchanganyia kwenye mlo, mpaka kula baada ya chakula.

Ikianziwa na juisi yake, mpaka inapoliwa kama tunda, mara nyingi inajulikana chakula chenye afya. Mtaalamu wa lishe aliyesajiliwa Taasisi ya Jo Lewin, ana ufafanuzi wake, akiwa na orodha ya faida.

FAIDA ZA PARACHICHI 

Sehemu yake ina mgawanyiko wa parachichi na una: protini gramu sita (6); mafuta gramu tano (5); wanga gramu sita (6); potasiamu miligramu 360; na Vitamini E, miligramu 56.

Faida zake zinagawanyika katika orodha kadha:

Kwanza, parachichi linatajwa kuwa chakula chenye virutubisho vingi. Parachichi, pia ni chanzo bora cha mafuta na ina Vitamini E ndani yake, ikiwa chanzo kizuri cha virutubishi. Pia, hutoa nyuzinyuzi nyingi zaidi kuliko matunda mengine, ndani yake kukiwapo madini muhimu kama chuma, shaba na potasiamu.

Pili, tunda hilo linatajwa kuwa na msaada kwa afya ya moyo, parachichi lina mafuta mengi huku asilimia 60 yakiwa ni asili, ambayo utafiti unapendekeza kusaidia kulinda magonjwa ya moyo na kupunguza shinikizo la damu. 

Tatu, ni chanzo bora cha potasiamu, virutubishi na nyuzi, ambavyo vyote hunufaisha moyo na mfumo wa moyo na mishipa. 

Inaweza kusaidia kupunguza lehemu inayotolewa na parachichi pamoja na asidi ya mafuta ya mbegu. Mafuta hayo ambayo hayajajazwa, hupendekezwa kama sehemu ya lishe bora kusaidia kudhibiti lehemu(cholesterol).

Nne, hilo parachichi linaweza kusaidia kudhibiti hamu ya kula, ikiwa na kalori nyingi zaidi kuliko matunda na mboga nyinginezo.

Hata hivyo, uchunguzi wa kuvutia umeonesha kuwa mafuta ya parachichi husababisha hisia za shibe ambayo husaidia kudhibiti hamu ya kula. 

Tano, zao hilo la parachichi linaweza kusaidia kuweka macho yenye afya kando na faida zilizotajwa hapo juu, ikiwa chanzo kikubwa cha Vitamini E ya kinga, pamoja kusaidia macho yenye afya. 

USALAMA WAKE

Baadhi ya watu wanaweza kupata mzio wa parachichi. Hii ni pamoja na mizio kwenye mdomo ambayo inaweza kusababishwa na athari za nadra. 

Parachichi, pamoja na matunda kadhaa ikiwamo matunda kama tufaha, yana kemikali za asili zinazoitwa ‘salicylates’. 

Baadhi ya watu wanaweza kupata athari ya mzio ikiwa ni pamoja na upele wa ngozi na uvimbe. 

·     Ni elimu ya habari, ambayo undani wake inapatikana katika vituo vya huduma za afya.

Kwa mujibu wa BBC.