Katavi, Rukwa zilivyoachiwa trilioni 1.246/-, rekodi ya uwekezaji tangu tarehe ya uhuru

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:27 PM Jul 26 2024
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoani Songwe.
Picha:Ikulu
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa katika mji mdogo wa Tunduma, mkoani Songwe.

IKIWA ni mwendelezo wa uchambuzi wa ziara ya wiki moja ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, pata Makala ya majumuisho ya uwekezaji mradi maendeleo ilivyo.

INAWEZA kuelezwa wiki kamili ya ziara yake, katika baadhi ya mikoa ya Kanda za Juu Kusini yakimaliza kwa kishindo cha maendeleo ndani ya wiki, katikati ya mwezi ulioko sasa, Julai, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akijipanga kimkakati.

Akiwa katika mikoa hiyo ya pembezoni mwa nchi, Katavi, Rukwa na Songwe alikomalizia safari, ni mikoa iliyokuwa na baadhi ya mapengo Rais akipigana  kuziba mapengo.

Alishiriki kufunga Wiki ya Wazazi Julai 13, 2024 mkopani Katavi kwenye Viwanja vya Azimio, baada ya hapo akaendeleza mfululizo wa uzinduzi wa uwekezaji wake, hasa wa miradi mikubwa.

Ikatamkwa mkoa wa Katavi umevunja rekodi ya kupata fedha nyingi za maendeleo serikalini, Mkuu wa mkoa wake, Mwanamvua Mrindoko, akikiri haujawahi kupata fedha nyingi za maendeleo kama inavyopata sasa, chini ya Rais Samia; Sh. Trilioni 1.246,776 (Sh. 1,246,776,000,000) za maendeleo. 

Mikoa aliyozuru iko juu katika uzalishaji zao kuu la mahindi, kwa mkoani Katavi, Rais Dk. Samia akipandisha bei ya mahindi ya wakulima kwa kilo kutoka Sh. 500 kwa kilo hadi Sh. 600 maeneo ya vijijini na 650 mijini.

Alipofika mkoani Rukwa Julai 17. 2024 akihitimisha ziara yake kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Manispaa ya Sumbawanga, nako akaongeza tena bei ya mahindi hadi Sh. 700, kutoka ya awali Sh. 500.

Hayo yanajiri, huku mkoa wa Katavi kwa sasa unakua kwa kasi katika utalii kwenye mbuga ya Katavi, Bandari ya Kale na ‘Center’ ya Mpanda, serikali imefanya maboresho kwenye ya Uwanja wa Ndege wa Mpanda, ambako alikagua ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja huo wa ndege, uliogharimu Sh. bilioni 1.4.

Mkoa wa Katavi ambayo tangu uhuru hakiuwaji kupata huduma ya umeme wa Gridi ya Taifa, imekuwa ikitumia wastani wa zaidi ya Sh. bilioni mbili kila mwezi kuwasha majenereta ya umeme. 

Mageuzi hayo ya Rais Dk. Samia kumetumika Sh. bilioni 48 kujenga kituo kikubwa cha kupoza umeme katika Grid ya Taifa, kilichoko Inyonga Mpanda, ambacho kitaufungua mkoa huo kupata umeme wa uhakika kihistoria.

Katia tafsiri ya mji Katavi kukua kwa kasi, ulinzi na mahitaji ya huduma za ulinzi na usalama wake umekuwa juu, kuchochea shughuli za kiuchumi. Hapo, Rais Dk. Samia, akazindua jengo la kisasa la makao Makuu ya  Polisi mkoani Katavi, hata kukaamsha shangwe kwa wananchi.

Upande wa kilimo cha Katavi, ni mkoa wa kilimo unaolisha taifa. Akiwa ziarani, Rais Dk. Samia alizindua maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhi nafaka vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Ofisi ya Wataalamu wa NFRA.

Vyote jumla vina uwezo wa kuhifadhi tani 25,000 kwa wakati mmoja, pia akazindua vipimo vya kisasa kupima mazao ya wakulima, pia kukashuhudiwa ziara kwenye hospitali ya rufani inayojengwa kwa awamu mjini Mpanda na inatumika sasa, iliyoainishwa katika gazeti hili Alhamisi wiki iliyopita.

MKOANI RUKWA.

Mkoani Rukwa, Rais Dk.,Samia akazindua mfululizo wa miradi ya maendeleo, huku mkoa huo ukipata fedha nyingi za maendeleo kiwango chake zikiweka rekodi katika historia ya mkoa huo.

Akikagua na kuzindua hospitali kubwa na ya kisasa, wilayani Nkasi iliyogharimu Sh. bilioni tatu na kunena lengo ni kuwafikishia karibu huduma wananchi, ambao walikuwa wanasafiri kwenda mjini Sumbawanga, takribani kilomitaa 100.

Pia, kukatangazwa serikali imetoa Sh. bilioni 4.5 za kujenga majengo ya kisasa ya Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, kwenye mji wa Matai, wananchi wasafiri mbali kwenda Sumbawanga kufuata huduma.

Hiyo ndio ikaendana na hatua ya Rais kuzindua barabara kubwa kiuchumi mpaka iliko Bandari ya Kasanga, ikiunganisha Sumbawanga- Matai- Kasanga yenye umbali kilomita 107 kwa gharama Sh. bilioni 150, matarajio baada ya uzinduzi ni kufungua uchumi wa mkoa Rukwa na majirani wa Zambia. 

Rukwa, kama ilivyo Katavi ni mkoa uliobobea katika kilimo cha mahindi na ndio zao kubwa la biashara. Huko nako Rais Dk. Samia alizindua maghala na vihenge vikubwa vya kuhifadhi nafaka na mazao yanayolisha taifa. 

Rais Dk. Samia alizindua maghala na vihenge hivyo,  ili kuongeza uwezo zaidi wa taifa kuhifadhi mazao kwa mauzo nje na matumizi wakati wa dharura vilivyogharimu Sh. bilioni 14 kijijini Kanondo, Sumbawanga, ili kuongeza uwezo wa taifa kuhifadhi mazao kwa mauzo nje na matumizi ya dharura.  Ni aina ya msukumo Rais anauweka, kukabiliana na dhana kwamba ‘ilisahaulika.’

Kwenye ziara yake hiyo, Rais Samia akazindua Chuo cha VETA kilichotumia Sh. Bilioni 6.08 kilichopo Kashai Sumbawanga mjini na kimeshaanza kutoa huduma ya kupika vijana kwa fani za ujuzi, pia akaweka katika Uwanja wa Ndege wa Rukwa uliofika asilimia 18.  

Vilevile, mkoani Rukwa akazindua  Chuo cha Ualimu Sumbawanga, pia akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Rukwa, kijijimo Mtindile, eneo la Laela. 

Rais Samia akaweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Kampasi ya Rukwa, kukidhi kilio cha miaka mingi wakitaka nao wawe na chuo kikuu. 

Mjini Sumbawanga, akaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kilomita sita, kwenda Seminari ya Kaengesa.

MKOANI SONGWE.

Katika eneo la transfoma ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Rais Dk. Samia akawasalimia wananchi ambako Mbunge wa Tunduma, David Silinde akaeleza jinsi mji mdogo wa Tunduma ulivyopaa kiuchumi, hata kujengwa miradi mikubwa ya maendeleo, akisifu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk. Samia.

Mbunge wa Viti Maalum mkoani Songwe, Stella Fiyao (CHADEMA), akasifu Serikali ya Awamu ya Sita, kwa ujenzi wa miradi mikubwa na midogo, ikiwamo muuganiko wa kisiasa, kati ya chama tawala CCM na CHADEMA.

Fiyao akatumia nafasi hiyo, kumuomba Rais Dk. Samia kuweka mazingira rafiki ya wafanyabiashara, akisema asilimia 75 ya maduka makubwa yaliyopo upande wa Nakonde nchini Zambia, yanamilikiwa na Watanzania ambao huenda wanakimbilia huko, kukwepa utitiri wa kodi miaka ya nyuma.

George Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi na Japhet Hasunga, Mbunge wa Vwawa mkoani Songwe kwa nyakati tofauti baada ya kupewa nafasi, hawakusita kusifu kazi ya serikali, huku Mbunge Hasunga akikazia ombi la mji wa Vwawa kufanywa Manispaa.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, naye akatoa nasaha zake, huku Rais Dk. Samia akiwa juu ya gari, alimuona kijana mwenye mlemavu akamwita na kumuagiza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kuhakikisha anamnunulia mguu bandia kwa fedha za ofisi yake.

·                       Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu: 0718 382817-0766936392 na barua pepe: [email protected]