Safari za treni ya umeme Dar - Dodoma zaanza rasmi

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 01:25 PM Jul 25 2024
Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza rasmi Safari za Treni ya Umeme kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma.Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa kabla ya kuanza safari hiyo akizungumza na. waandishi wa habari amesema muitikio umekuwa mkubwa wananchi wanaotumia usafiri huo ambapo zaidi ya abiria 900 wamesafiri kuelekea Dodoma.