PSSSF yatoa msaada kwa hospitali tatu na watoto wenye mahitaji maalum

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:16 AM Oct 12 2024
PSSSF yatoa msaada kwa hospitali tatu na watoto wenye mahitaji maalum
Picha:Mpigapicha Wetu
PSSSF yatoa msaada kwa hospitali tatu na watoto wenye mahitaji maalum

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula kwenye hospitali tatu za Rufaa za Mikoa wakiwemo watoto wenye uhitaji maalum. Misaada hiyo ambayo imetolewa katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, ni sehemu ya kusaidia jamii kutokana na pato la Mfuko.

Hospitali ambazo zimefaidika na misaada hiyo ya PSSSF, ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Meneja wa Pensheni za Wastaafu PSSSF, Kwame Temu ndiye aliyewasilisha msaada huo maalum kwa wodi ya watoto wenye changamoto ya Lishe.


Kwa upande wa Mkoa wa Arusha, Meneja wa Kumbukumbu za Wanachama Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Edgar Shumbusho, yeye alimkabidhi vifaa tiba, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), Dk. Alex Ernest.

Wakati Meneja wa PSSSF Mkoani Mtwara, Say Lulyalya, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mgtwara, Abdallah Mwaipaya, katika hafla iliyohudhuriwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa, Ligula.


Aidha, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Morogoro, Zaida Mahava, yeye alikabidhi vifaa vya ujenzi na vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege mkoani humo.