Waziri Kikwete atembelea Banda la PSSSF Wiki ya Vijana Mwanza

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:27 PM Oct 11 2024
Waziri Kikwete atembelea Banda la PSSSF Wiki ya Vijana Mwanza
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri Kikwete atembelea Banda la PSSSF Wiki ya Vijana Mwanza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, akipewa maelezo na viongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Paul Kijazi, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana, kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Oktoba 11, 2024.

PSSSF inashiriki ili kutoa huduma na pia elimu ya hifadhi ya Jamii ikiwemo fursa za uwekezaji.

Vijana 1,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini wanashiriki katika wiki hiyo ambapo pamoja na kutembelea maonesho mbalimbali lakini pia watapata uelewa wa fursa za ujasiriamali, ubunifu wa kidijitali katika kujifunza na kujiajiri sambamba na elimu ya Sera mpya ya maendeleo ya vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024.