CP Hamadi: Ruksa kula mchana Ramadhani, tulikamata wavuta bangi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:59 PM Apr 02 2024
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad.
PICHA: MAKTABA
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad.

KAMISHNA Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad, amesema hakuna sheria inayowaruhusu Polisi Zanzibar kuwakamata watu wanaokula hadharani mchana wakati wa Ramadhani, na kusema kuwa chanzo cha msako uliofanyika ni baada ya video iliyowaonesha watu wakivuta bangi mchana maeneo ya Maisara Zanzibar.

CP Hamad ametoa ufafanuzi huo kufuatia operesheni iliofanyika Mkoa wa Mjini na kuwakamata watu waliodaiwa kula mchana wa Ramadhan “Hakuna sheria inayokataza watu wasile mchana wa Ramadhani, nilitoa maelekezo baada ya video ya wanaovuta bangi kwamba ifanyike oparesheni wale wavuta bangi kwasababu bangi ni kosa la jinai hakuna sheria inayoruhusu watu kuvuta bangi ila hatukuwakamata wala mchana”

“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mamlaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili zifanyike kwa usalama na amani”

“Kwa sababu bangi haijaruhusiwa Zanzibar, nilimpa taarifa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi ambaye ndio mwenye himaya hiyo na kumpa maelekezo washughulikie tatizo hilo kwasababu, watu kama wanakaa mchana wanavuta bangi wanaona kama sisi hatupo,” amesema.