Clemence adaiwa kujaribu kumuua mama yake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:02 PM Apr 03 2024
Kijana akiwa na mawazo.
PICHA: MAKTABA
Kijana akiwa na mawazo.

CLEMENCE Maela mkazi wa mtaa wa Yombo Matangini kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam, anatuhumiwa kujaribu kumuua mama yake mzazi na yeye kujaribu kujiua baada ya watu kuhisi amemuua mama yake.

Tukio hilo alilitekeleza Jumapili ya Pasaka ambapo baada ya kumjeruhi mama yake aliupakia mwili wake kwenye bodaboda na kwenda kuutupa Buza maeneo ya Sigara ambapo siku ya Jumatatu mama yake aliokotwa akiwa hana nguo huku amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili.

Majirani wanasema walianza kumtilia shaka kijana huyo siku ya Jumamosi baada ya kusikia kelele za mwanamke akilia ndani ambapo baadae walimuuliza akasema kuwa ni mwanamke wake ameshaondoka hivyo wasiwe na wasiwasi.