Wakenya waguswa na picha za watoto wa Gachagua

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:58 PM Oct 18 2024
Wakenya waguswa na 
picha za watoto wa
 Gachagua
Picha:Mtandao
Wakenya waguswa na picha za watoto wa Gachagua

Watoto wawili wa Rigathi Gachagua, ambaye Bunge la Seneti limemvua madaraka ya Unaibu Rais wa Kenya, wameleta mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zao kunaswa wakionesha huzuni huku wakiwa hospitalini alikolazwa baba yao.

Vijana hao, Kevin na Keith, wakiwa na sura za huzuni, walionekana wakifuatilia hali ya baba wakiwa na huzuni kubwa mithili ya watu waliofiwa.

Jana mchana wakati shauri lake likiwa linajadiliwa mbele ya Seneti, Gachagua, 59, alipatwa na maumivu makali ya kifua ghafla na kukimbizwa hospitalini ambako hali yake imeelezwa inaendelea vizuri lakini bado anaangaliwa na madaktari.

Picha hizo zimewagusa Wakenya wengi huku baadhi wakiitumia familia hiyo ujumbe wa kuwatia moyo na kuwataka wamshukuru Mungu kwa kila jambo.