Mzee wa miaka 63 aoa binti wa miaka 12

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:48 AM Apr 02 2024
Ndoa.
PICHA: MAKTABA
Ndoa.

KIONGOZI wa Kitamaduni nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 63, ameripotiwa kuoa binti mwenye umri wa miaka 12, jambo ambalo limezua ghadhabu miongoni mwa watu nchini humo.

Kiongozi huyo wa kitamaduni aliyefahamika kama Nuumo Borketey Laweh Tsuru amemuoa msichana huyo katika sherehe ya kitamaduni iliyofanyika Jumamosi nchini humo. 

Unaambiwa umri wa chini kisheria wa kuoa nchini Ghana ni miaka 18 na kiwango cha juu cha ndoa za utotoni kimepungua, licha ya ndoa hizo kufanyika. 

Video na picha za tukio hilo la Jumamosi ambalo lilihudhuriwa na makumi ya wanajamii zimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, na hivyo kuzua kilio miongoni mwa Waghana wengi.